Ni sababu chache zinazoweza kumfanya mtu kupata virusi vya covid 19 hata baada ya kuchanjwa.
Ripoti zinasema kuwa chanjo za moderna na pfizer zina asilimia 95 ya uwezo wa kumkinga mtu, hii ina maana kwamba asilimia 5 ya wanaopewa chanjo bado wanaweza kuambukizwa virusi hivi
Uwezekano wa kulazwa hospitalini au kifo kwa aliyepata chanjo ni wa chini mno ikilinganishwa na ambaye hajachanjwa
Baada ya mtu kupewa chanjo humchukua muda ili kupata kinga inayostahili mwilini na huchukua wiki mbili zaidi ili awamu ya pili ya dozi ya chanjo aina ya moderna kutolewa huku siku 7 kwa dozi ya pili ya pfizer.
Vipimo vya uwezo wa chanjo za covid 19 zinazotolewa na makampuni ya dawa hazitoi picha kamili ya nguvu za chanjo hizo.kutokana na jambo hilo asilimia 5 ya wanaosemekana kuambukizwa virusi hata ingawa wamepokea chanjo yaweza kuwa watu tofauti.
Hakuna chanjo bora zaidi ya nyingine ila kuna sababu zinazochangia kwa chanjo hizi kutofanya kazi ikiwemo kinga ya chini mwilini
Kuna uwezekano mkubwa kuwa visa visivyo vya kweli vya maambukizi vinavyoripotiwa kuchangia kwa idadi ya wale waliochanjwa na baadaye kupatikana na virusi hivi.
Maafisa wa afya ya umma wanashauri kuvaa barakoa/maski na kuzingatia umbali na mwenzako hata ikiwa umepata chanjo ili wale ambao hawajachanjwa wawe salama na hata virusi visisambae zaidi.