Bei ya Bidhaa muhimu kama vile mkate na maziwa huenda ikapanda iwapo mswada unaopendekezwa na wizara ya fedha utapitishwa bungeni .
Bidhaa hizo zinatarajiwa kupanda kwa asilimia 16 huku mkate unaouzwa kwa shilingi 50 kwa sasa ukitarajiwa kupanda hadi shilingi 58.
Wenye mikopo pia wanatarajiwa kugaramika zaidi mswada huo ukipendekeza wanaochukua mikopo kulipia asilimia 20 kama faida
Kulingana na washikadau, hatua hiyo imesababishwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini katika siku za hivi karibiuni.