Mahakama Kuu ya Milimani imetupilia mbali amri ya kaimu inspekta jenerali wa polisi Douglas Kanja ya kupiga marufuku maandamano katikati mwa jiji la Nairobi.
Shirika la Katiba institute liliwasilisha kesi ya dharura likitaja kuwa naibu inspekta jenerali hana mamlaka ya kupiga marufuku maandamano hayo kikatiba.
Douglas Kanja ameeleza kuwa ripoti za kijasusi zinaashiria wahuni huenda wakatumia pengo kwenye maandamano kuharibu na kupora mali.
Aidha watetezi wa haki za binadamu wamekuwa mstari wa mbele kupinga ukatili unaotekelezwa dhidi ya waandamanaji huku wakiwalaumu maafisa wa polisi kwa kutumia risasi na nguvu kupita kiasi wanapodhibiti waandamanaji nchini Kenya.