Kutokana na mkurupuko wa janga la Covid19, mamia ya familia zinazoishi na ugonjwa wa seli tundu yaani sickle cell barani Afrika zinapata ugumu wa kupata dawa Pamoja na huduma zingine muhimu za matibabu ili kusaidia kudhibiti hali zao za kiafya.Hali hii imesababisha wengi kupoteza Maisha hasa Watoto na vijana wadogo .
Hata hivyo, katika mtaa wa Kibera nchini Kenya, vijana wenye umri kati ya miaka 14 na 22 wanaoishi na sickle cell, wameunda shirika lao ili kuwasaidia kupata fedha za kununua dawa Pamoja na na kugharamia matibabu mengine . Mwandishi wetu Victor Moturi, aliwatembelea vijana hao na kutuandalia taarifa ifuatayo.