Connect with us

News

Douglas Kanja Kiricho Kuhudumu Kama Inspekta Jenerali Wa Polisi

Published

on

Inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome amejiuzulu. Yanajiri siku moja baada ya Rais William Ruto kuvunja baraza lake la mawaziri.Koome amejiuzulu huku vikosi vya polisi vikilaumiwa kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu, utekaji nyara na mauaji ya waandamanaji.

Baada ya kujiuzulu kwa Koome,rais William Ruto alimteua Douglas Kanja Kiricho kama mshikilizi wa afisi ya inspekta jenerali wa polisi huku bunge likitarajiwa kupiga msasa uteuzi wake.

Kutoka mwaka wa 2018, Douglas Kanja alihudumu kama kamanda wa kikosi cha GSU.Akihudumu kwenye kitengo hicho,alishughulikia maswala ya dharura, kudhibiti usalama na kuongoza oparesheni kadhaa ikiwemo dhidi ya pombe haramu na dawa za kulevya.

Douglas Kanja aliwai kuhudumu kama mkurugenzi wa idara ya upelelezi nchini Kenya,DCI.

 

Imwene Daniel
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *