Connect with us

Habari

WORLDCOIN YAZUA TUMBO JOTO NCHINI

Published

on

Photo courtesy of Odhiambo Ogola (@PhilipOgola on Twitter)

Uchunguzi ulioanzishwa kupitia wizara wa usalama wa ndani na idara ya serikali ya kulinda data umeonyesha kwamba mfumo wa ukusanyaji wa  data kupitia jicho ulioanzishwa na kampuni ya Wold Coin ni hatari kwa wakenya.

Naibu Kamishna katika idara hiyo Oscar Otieno katika hati  kiapo aliyowasilisha mahakamani alidai kwamba operasheni hiyo ni hatari kwa Wakenya na uchunguzi zaidi unaendelea.

Oscar vilevile alidai kuwa mfumo huo wa World coin ulitumika kupata taarifa za siri kuhusu wakenya na kunauwezekano wakutumia kwa njia isiyofaa.

Wiki mbili zilizopita maelfu ya wakenya walipiga foleni katika maeneo mbali mbali ikiwemo Jumba la KICC wakisubiri kusajiliwa kwa njia ya jicho na kampuni hiyo ya World coin.

Oparesheni hiyo ilikatizwa baada ya waziri wa usalama wa ndani Prof Kithure Kindiki kuonyesha wasiwasi wake na data iliyokusanywa na kampuni hiyo.

Charity Kilei
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *