Katika kipindi cha miezi miwili ijayo wizara ya utalii itaongoza huduma ya kuwahesabu Wanyama katika mbuga za humu nchini.
Kulingama na waziri wa utalii Najib Balala,zoezi hilo litawezesha serikali kujua idadi kamili ya Wanyama pori waliomo nchini Pamoja na majini na vile vile kusadia kuweka mikakati mwafaka Pamoja na sera za kitalii ili kupiga jeki sekta hiyo .
Kwa mujibu wa Balala,idadi ya Wanyama hasa wale walio kayika Hatari ya kuangamizwa inafaa kuangaziwa Zaidi kupitia sheria za Wanyama pori mwaka 2013. Waziri huyo ameongeza kuwa Kenya haijawahi kuwa na zoezi kama hili .
Kwa upande wake mkurugenzi wa Shirika la huduma ya Wanyama pori nchini Brigedia John Waweru amewahakikishia wakenya kuwa huduma hiyo itafanywa kwa utaalam wa hali ya juu.
’’Raslimali zilizotengwa na serikali kupitia wizara ya utalii na Wanyama pori zitatumika vyema kwa mujibu wa sheria zilizowekwa’’Alisema Waweru.