Watumishi wa umma huenda wakapokea nyongeza ya mishahara chini ya miezi mitatu ijayo , amesema waziri wa utumishi wa umma Aisha jumwa.
waziri huyo amesema kamati maalum itaundwa kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu mbinu mwafaka itakayotumika kutekeleza nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi hao.
Ni mpango ambao , kulingana na jumwa, unalenga kupunguza visa vya ufisadi serikalini. Amesema ikiwa wafanyakazi wa umma watalipwa vizuri, huenda kusishuhudiwe visa vya ufisadi siku za usoni.
Haya yanajiri huku hazina ya kitaifa ikihangaika kutimiza matakwa ya wafanyakazi wa umma ya nyongeza ya mishahara. Hivi maajuzi, maseneta walitishia kumbandua afisini mkuu wa tume ya kutathmini mishahara ya wafanyikazi wa umma nchini (SRC) lynee Mengich kwa kupunguza mishahara na marupurupu yao.
Tangazo la Jumwa linajiri huku shirika la fedha ulimwenguni (IMF) likiishinikiza serikali ya rais William Ruto kupunguza mishahara ya watumishi wa umma ili kutenga fedha za kukamilisha miradi ya maendeleo humu nchini.
Imehaririwa na Henix Obuchunju