Ongezeko la magonjwa kama vile saratani na kisukari husababishwa na ulaji wa vyakula vilivyo na kemikali nyingizi kutoka dawa zinazotumiwa kuwaua wadudu wanaoshambulia mimea.
Haya yamejiri Katika mkutano ulioandaliwa na shirika la Heinrich Boll Stiftung hapa Nairobi kujadili mbinu za kupunguza matumizi ya dawa hizo ambazo zimepigwa marufuku Umoja wa Mataifa.
Shirika la Stiftung linashikilia kuwa matumizi ya dawa hizo barani Africa inachangia pakubwa ongezeko la magonjwa hayo huku akiitaka ya Kenya serikali kumakinika.
Dk.Kimani Ngaruia kutoka Stiftung amedokeza kuwa tayari mswada wa kujadili dawa hizo umewasiliswa bungeni na kuwarai wabunge kuunga mkono pale utakapoanza kujadiliwa.
Baadhi ya vyakula ambavyo vimesekena kuwa na kemikali nyingi ni Sukuma wiki, Nyanya na Mahindi.Hivi, kulingana na wataalam, ni vyakula vinavyoliwa na mwananchi wa kawaida na ipo haja ya hatua ya dharura kuchukuliwa.