Huku ulimwengu unaposherehekea siku ya uhuru wa vyombo vya Habari ,Idara za serikali nchini Kenya zimepongeza juhudi za wanahabari katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika sekta hiyo.
Spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi amewarai wanahabari kuzingatia Habari za kweli kabla kuchapisha au kuzipeperusha ili kutoupotosha umma.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na baraza la vyombo vya Habari nchini (MCK) ,Muturi aliwaomba wamiliki wa vyombo vya Habari kushughulikia maslahi ya wanahabari hasa malipo duni wanayopokea.
Kwa upande wake katibu wa kudumu katika wizara ya Habari na mawasiliano,Esther Koimet alisema serikali ina mipango ya kutenge fedha zitakazoimarisha na kuendeleza sekta ya uandishi wa Habari nchini,ili wakenya kupokea Habari muhimu kwa haraka.
Tarehe 3 mwezi wa Mei huadhimishwa kila mwaka kama siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari nchini.