Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko amejitetea dhidi ya taarifa kwamba tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini (EACC ) inatilia shaka alikotoa mali ya mabilioni ya pesa anayomiliki.
Kupitia mtandao wa Twitter , Sonko amesema kumiliki mali humu nchini si makosa na kwamba kunyamaza kwake hakupaswi kutafsiriwa kuwa ujinga.
Gavana huyo wa zamani alikuwa akizungumza baada ya EACC hapo jana kutangaza kuwa inawachunguza waliokuwa magavana Evans Kidero(Nairobi) Ferdinand Waititu (Kiambu) Mike Sonko (Nairobi) Pamoja na gavana wa sasa wa Samburu Moses Lenolkulal.
Tume hiyo inadai magavana hao wamefuja shilingi billion 11.5 ambazo ni mali ya umma. Sonko na Waititu walitimuliwa afisini kwa tuhuma za ufujaji wa mali ya umma miongoni mwa sababu zingine.
Kidero alishtakiwa na EACC kwa tuhuma zizo hizo huku tume hiyo ikishikia kuwa gavana huyo wa kwanza wa Nairobi anafaa kurudushishia kaunti ya Nairobi Zaidi ya bilioni 10 ambazo alidaiwa kufuja.