Connect with us

Habari

Shirika La Spurgeon Yasherekea Miaka 20!

Published

on

PICHA KWA HISANI YA WANACHAMA WA SCCK.

Shirika la Spurgeon child care Kenya limesherekea miaka 20 ya kuhudumu  eneo bunge la Kibra.

Spurgeon ni shirika ambalo hujihusisha na kusaidia wanafunzi ambao wanatoka katika mazungira magumu kwa kuwapa masomo na chakula, jambo ambale wamejishughulisha najo kwa zaidi ya miaka ishirini sasa.

Kando na hayo shirika hilo limeungana na washikadau kutoka uingereza ambapo wao hupata ufadhili ili kutekeleza majukumu yao.

Sherehe hilo limeandaliwa katika shule ya Spurgeons katika eneo bunge la Kibra ambapo vilevile wazazi na watoto walihudhuria. Aidha bodi inayosimamia shule hio wakiwemo Mkurugenzi Wilchyster Maseno, Mkurugenzi anayesimamia oparesheni Kenyanito Dudi pamoja na Mwenyekiti Vicky Odhiambo walihudhuria na kuzungumza na wenyeji.

Vilevile, aliyekuwa seneta wa Kisumu Fred Outa ambaye pia ni msaidizi wa shughuli mbalimbali katika shirika hilo , alikuwa mmoja wa wageni waalikwa.

Kwa taarifa zaidi sikiza ripoti iliyoandaliwa hapa chini.

Henix Obuchunju
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *