Tangu kuanzishwa kwa zoezi la chanjo dhidi ya virusi vya korona humu nchini,kumekuwa na dhana potovu kuhusu chanjo hiyo hasa katika mitaa ya mabanda.
Dhana hizo ni kama vile kukosa nguvu za kiume, kupoteza uwezo wa kuona na kadhalika.
Licha ya hayo, baadhi ya wenyeji wakishirikiana na mashirika mbalimbali wamekuwa wakielimisha umma kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo mtaani kibra.