Siasa za azimio la umoja zinatarajiwa kuelekea katika kaunti ya Homabaya hapo kesho agosti 19, 2021 baada ya kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila odinga Kutangaza hapo jana.
Bw Odinga anatarajiwa kukutana na viongozi kutoka kaunti zote za eneo la nyanza Kisumu, Nyamira, Kisii, Siaya , Migori na Homabay . Ni mkutano ambao utandaliwa eneo la Oyugis katika kaunti ya Homabay
Kulingana na Wakili ken omondi ni kuwa chama cha Odm bado kinasalia kuwa dhabiti katika eneo la Nyanza .
Bw odinga anatarajiwa kuelekea Katika eneo la magaribi mwa Kenya siku ya Ijumaa Agosti 20, 2021 siku ambyao mahakama inatara jiwa kutoa uamuzi wake kuhusiana na kesi iliyowasilishwa mahakamani kupinga mchakato wa bbi .
Kunatarajiwa pia kuwepo na mungano wa kisiasa baina ya chama cha Jubilee na chama cha Odm
“ Moja ya maswala ambayo yako wazi sasa hivi ni kuwa kwa wakati huu tunatarajia mazungumzo ya mungano “ amesema wakili omondi ambyae pia ni mwanasisasa eneo la Kisumu .
Katibu mkuu wa chama cha jubilee Raphael tuju akihuhutubia wandishi wa habari Agosti 17 , 2021 alisema kuwa kamati ya chama cha jubilee kimempa idhini ya kufaya mazungumzo vya vingine pia vya kisiasa kama vile Wipper , Anc na KANU.