Mkurugenzi wa shirika la Bridget Connect consultancy Bob Ndolo aliwasilisha ombi la kutaka mtandao wa kijamii wa Tik Tok kupigwa marufuku nchini Kenya kwa madai ya kusambaza picha za ngono na matumizi ya lugha ya matusi.
Tik Tok ni mtandao wa kijamii ambayo inamilikiwa na kampuni ya Uchina, ilipaata umaarufu sana duniani wakati wa COVID 19. Wakenya wengi walikumbatia apu hii kwa sababu ya ucheshi wake.
Tik tok inaumarufu sana hasa miongoni mwa vijana ambao wamepata ajira kwa utumizi wake. Ila baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa dini na wazazi wanalalama dhidi ya athari ya utumizi wa apu hii.
Katika mawasilisho hayo ndolo amedai kwamba vijana wanaathirika kwani ni waraibu sugu wa kutumia Tik Tok
Ombi hilo limewasilishwa bungeni na wambuge wanatarajiwa kujadili na kutathmini hatma yake.