Kinara wa chama cha ODM Bw Raila odinga hatimaye ametangaza kuwa atawania kiti cha urais mwaka ujao . Odinga ameyasema haya kwenye uwanja wa michezo wa kasarani jijini Nairobi katika hafla iliyohudhuriwa na maelfu wa wafuasi wake .Bw Odinga kwenye hotuba yake alizindua nguzo muhimu ambazo serikali yake itaangazia ikiwa atachaguliwa kuwa rais wa tano wa taifa la Kenya .
“INUA JAMII PESA KWA WOTE ” kwa mujibu wa Odinga ni mpango utakaowezesha wakenya maskini kupokea shilingi elfu sita kila mwezi .
“KAZI KWA WOTE “, “UCHUMI KWA AKINA MAMA” ni mpango utakaowawezesha vijana kuwa na maarifa na ujuzi wa kiteknologia .
“WASTE NO SINGLE CHILD” ni programu ambayo itawezesha watoto kupata elimu bora huku “ FUKUZA NJAA”ukiwezesha uzalishaji bora nchini .
“ONE COUNTY ONE PRODUCT” ni mpango utakaowezesha uzalishaji wa mali ya Kenya na kutumika humu nchini na bidha zingine kusafirishwa au kuuzwa nje ya nchi
“ BABACARE” ni mpango utakaowawezesha wakenya kupokea shughuli zote za matibabu pahala popote nchini pasi na changamoto.
Viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla hiyo wametangaza k.umunga mkono Bw Odinga huku Bw S.K Macharia ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Royal Media akisema kuwa kuunga mkono Bw Odinga ni uamuzi wake wa kibinafsi ila sio msimamo wa kampuni anazomiliki