Familia moja katika eneo la kayole jijini Nairobi inalilia haki baada ya binti yao wa miaka 8 kufa katika katika hali isiyoeleweka.
Mwili wa mwanafunzi huyo darasa la 2, Jennifer Michelle, ulipatikana na wazazi wake katika hospitali ya mama lucy baada ya kutafutwa kwa saa 5.
Kwa mujibu wa wazazi, haileweki ni vipi mwili wa mtoto huyo ulivyofika katika hospitali ya mama lucy.
Hapo jana wazazi wa jennifer michelle wanasema walimwandaa kwenda shule kama kawaida, bila kujua kwamba hatarudi nyumbani akiwa hai tena.
Wazazi hao wanadai mwanao alikuwa na afya njema, na mwenye furaha alipofikishwa katika lango la shule na mama yake. Uchunguzi kuhusu kifo cha Jennifer unaendelea.