Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi amekariri kuwa kuna umuhimu wa taasisi zinazohusika na kubuni sera zinazoangazia utozaji ushuru kwa wakenya na biashara humu nchini kujumuisha maoni na malengo ya wakenya kwenye ubunifu wa sera hizo ili kuwapa afueni wakenya na wafanyi biashara kwenye harakati zao za kupiga jeki uchumi na mapato ya taifa hili.
Mudavadi akizungumza kwenye kongamano lililoandaliwa na halmashauri inayosimamia masuala ya wafanyibiashara na makampuni, KNCCI amesema ushuru unaotozwa wakenya na wafinyibiashara ni sharti uwe wa kiwango kinachoweza kuwafanya kuwa na salio la mapato ambayo wanaweza ekeza kama akiba.
Mudavadi amesisitiza umuhimu wa sekta kuu za serikali zinazotoa huduma muhimu zinazochangia ustawi wa biashara kuzidisha juhudi zake ili kutoa nafasi kwa halmashauri ya utozaji ushuru nchini KRA, kuwa na wakati mwepesi wa kutimiza malengo yake bila ya kuwakandamiza wafanyibiashara na wakenya kwa jumla .
https://pamojafm.co.ke/habari/mudavadi-azungumzia-uamuzi-wa-mahakama-kuhusu-bbi/
Mudavadi pia amegusia suala la bei ghali ya kawi na bidhaa zinazotokana na kawi ikiwa ni Pamoja na petroli, mafuta taa na Stima(Umeme) kuwa mojawepo ya chanzo cha kusambaratika kwa viwanda vya ukuzaji na uzalishaji nchini .
Kiongozi huyoa amesisitiza kuna umuhimu mkubwa kwa majadiliano ya kina kuhusiana na suala zima la ushuru huku akiwataja wafanyibiashara wa kiwango cha chini kama akina mama mboga ambao pia wanajitahidi kujimudu kimaisha kama mojawepo ya wakenya wa hadhi ya chini ambao mzigo mkubwa wa ushuru huwaangukia huku mapato yao yakiwa ya chini mno.