Ijapokuwa bado ushirikina haujafafanuliwa kwa ujumla maana yake inamaanisha imani katika nguvu zisizo za kawaida .
Imani za ushirikina zimeonyeshwa kusaidia kukuza mtazamo mzuri wa kiakili katika mwili wa mwanadamu.
Ingawa wakati mwingine zinaweza kusababisha maamuzi yasiyo na mantiki, kama vile kuamini sifa za bahati nzuri na hatima badala ya kufanya maamuzi msingi.
Kuvalisha watoto hirizi, kuvaa nguo fulani, kutofagia usiku ,kuvaa nguo za rangi maalum na kutumia nambari fulani ni mambo yanayo usishwa na ushirikina.
Na ingawa tabia na vitendo hivi vinaweza kuonekana kuwa vya kawaida, kwa watu wengine, mara nyingi vinaweza kuathiri chaguzi zinazofanywa katika ulimwengu wa kisasa.
Edna kalata na taarifu hiyo kikamilifu.