Mfanyabiashara Tom Mboya amehukumiwa kifungu cha miaka 23 jela kwa kupatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumjeruhi miliki wa mgahawa wa Ranalo Foods Bw William Osewe .
Ni uamuzi uliofanywa na Jaji Martha Mutuko wa mahakama ya Milimani Jumatano 6/10/ 2021.
Kwenye mahakama ya Milimani ,“Nimetizama ripoti iliyowasilishwa mbele yangu na kunakili kuwa mshtakiwa , Tom Mboya hajajutia kwa lolote lile kutokana na kitendo alichofanya “ alisema jaji Martha
Mahakama pia ilirejelea dhana kuwa mshtaki Osewe aliathirika na bado kufikia sasa ana madhara ya kupigwa risasi
“Namhukumu mshtakiwa kwa miaka 20 jela kwa kujaribu kutekeleza mauaji na miaka mitatu kwa kujeruhi “ alisema jaji Mutuku.
Bw Mboya anadaiwa kumpiga risasi mara kadha Bw Osewe Mwezi Disemba mwaka wa 2016 katika eneo la Garden Estate eneo bunge la kasarani walipokuwa na mzozo kuhusu mwanamke anayefahamika kwa jina Bi Stella Mutheu
Bw Osewe alilazwa kwenye hospitali ya Aga Khan ambapo alifanyiwa upasuaji kadha ili kuondoa risasi alizokuwa amepigwa .
Bw Mboya alijisalimisha kwenye kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani alipojitetea dhidi ya mashtaka mwaka wa 2017 na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi Ksh 300,000