Waziri wa elimu Prof. Goerge Magoha amekana madai kuwa matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE ya mwaka jana yapo tayari.
Waziri huyo amesema matokeo hayo yatatangazwa pale alama za wanfunzi hao katika Masomo yote zitakapojumulishwa.
Akizungumza katika shule ya upili ya Starehe baada ya kushuhudia kukamilika kwa usahihishaji wa mtihani huo, waziri Magoha amesisitiza kuwa shule zitafunguliwa juma lijalo ila wanafunzi wa Grade 4 watatakiwa kusalia nyumbani hadi Julai 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Magoha, hilo imesababishwa na taratibu za mtaala mpya ambazo zilianza kutekelezwa miezi kadhaa iliyopita.