Connect with us

Habari

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Published

on

Dunia huadhimisha siku ya UKIMWI  kila mwaka,mwezi wa Disemba tarehe 1. Ni siku ya kuwakumbuka wote waliopoteza maisha yao na pia kuonyesha mshikamano na watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI  (HIV) pamoja na  kuelimisha, kupima na kuondoa unyanyapaa katika jamii.

Mwaka wa 2022 , shirika la afya (WHO) lilitumia kauli mbiu ya  “Equalize” ikisisitiza umuhimu wa usawa katika upatikanaji wa huduma za afya na kuzuia Ukimwi. Hii ilihamasisha watu kutafuta njia za kuhakikisha kila mtu anapata habari na rasilimali zinazohitajika. Kwa mwaka huu, WHO inatualika kufikiria juu ya jinsi jamii zetu zinavyoweza kuongoza katika mapambano dhidi ya Ukimwi kwa mada “Let communities lead”.

Akizungumza na kituo cha Pamoja FM Daktari Anthony Njoroge, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza, anaeleza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni wito kwa wanajamii kuchukua jukumu kuwasaidia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Anasema kuwa jamii inapaswa kuchukua hatua ili kusaidia wanaoishi na virusi vya hivi.

“Jambo la muhimu  ni  jamii iwe na uwezo wa kuwashughulikia wagonjwa, isiwe wahudumu wa afya  pekee  ndio wana uwezo wa  kutoa usaidizi. Pia jamii iwashauri, kuwahimiza na kusimama wa wanaoishi na virusi hivi.Aidha wanajamii wawe mstari wa mbele kuondoa unyanyapaa kwa wagonjwa wa virusi vya UKIMWI.

Daktari Njoroge anaendelea  kusema kuwa wanajamii wanafaa kuhakikisha kuwa wagonjwa hawa wanakula vizuri na hawatumii madawa ya kulevya kwa vyovyote vile.

“Usije ukamwona yule mwathiriwa wa virusi vya UKIMWI anastahili kufa. Virusi hivi vimekuwepo tangu wakati wa maumbile na havina tiba. ”

Daktari anasisitiza kuwa  kauli mbiu ya mwaka huu “Let communities lead” inatukumbusha kuwa nguvu zetu kwa pamoja zaweza kuleta mabadiliko. Tuwe kila mmoja wetu sehemu ya suluhisho na kusimama pamoja dhidi ya UKIMWI.

Wendy Wangui
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *