Mzozo baada ya uchaguzi unasemekana kuwa donda sugu barani Africa. Kila baada ya chaguzi kuu, nchi nyingi hujikuta kwenye kipindi cha mzozo huku upinzani katika mataifa hayo ukipinga matokeo ya uchaguzi.
Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa (United Nations) Katika machafuko ya uchaguzi wa 2007 nchini Kenya zaidi ya watu 1200 walipoteza maisha huku zaidi ya wa 300,000 walipoteza makazi.
Baada ya uchaguzi wa Agosti 9,2022 nchi ya kenya ilijikuta kwenye machafuko ya baada ya uchaguzi mrengo wa upinzani Azimio la umoja ukipinga matokeo hata baada ya ya mahakama ya juu kutangaza Kenya Kwanza kama mshindi.
Mrengo wa upinzani uliandaa maandamano kote nchini hali ambayo ilisababisha vifo , uharibifu wa mali na kuzorota kwa hali ya uchumi.
Kwa muda, mrengo wa upinzani na serikali ya Kenya Kwanza walirushiana cheche za matusi na kujipiga vifua ila utulivu ulirejea kote nchini baada ya farasi wawili kuamua kushiri mazungumzo ya pande mbili.
Rais William Ruto ambaye hapo awali alikataa kushirikiana na Kinara a Azimio la umoja Raila Odinga ameonekana kulegeza kamba baada ya kuonyesha dalili ya kuunda kisheria afisi ya kiongozi wa upinzani.
Rais Ruto na Odinga kwa miezi hawakuweza kuonana ana kwa ana lakini sasa wanasalimiana na kualikana kwenye sherehe rasmi za kiserikali hata kabla ya mzungumzo ya pande mbili kukamilika.
Wakenya wengi walishiriki maandamano wakitaka gharama ya maisha kurudi chini lakini miezi michache baada ya maandamano kusitishwa gharama ya maisha haijashuka kwa mujibu wa wadadisi.
Naibu wa rais Rigthi Gachagu kwa upande mwingine ameonekana kutoridhika na maridhiano yanayoendelea kati ya Upinzani na Serikali akisistiza baadhi ya vipenge vilioko katika mazungumzo ya pande mbli kama kufanyia sava uchunguzi haipswi kuwa katika mazungumzo kwani matokeo ya uchaguzi uliidhinishwa na tume ya uchaguzi na mahaka ya juu.