Kenya inatarajiwa kupokea dozi milioni 1.7 za Modena na dozi 390,000 za johnson & johnson wiki ijayo ya Agosti 23, 2021.
Waziri wa afya mutahi kagwe akizungumza Jumatano Agosti 18,2021 amesema kuwa taifa pia linatarajiwa kupokea dozi zingine za Pfeizer katikati ya mwezi septemba mwakani.
Bw . kagwe pia amehimiza wakenya kupoke chanjo ya virusi vyaa corona kwani ni mojawapo ya kinga inayosaidia kudhibiti virusi vya corona
“Chanjo ni mojawapo ya kinga inayosaidia kukinga virusi vya corona “amesema waziri kagwe
Hili linakuja bada ya serikali kupokea dozi za 407, 000 za astrazeneka kutoka nchini uingereza na kupokelewa na Mkurugenzi wa afrya Patrick Amoth kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta .
Hii ikiwa ni mojawapo ya mipango ya serikali ya kuchanja watu milioni 26 ifikiapo Juni mwaka ujao na watu milioni 10 kufikia mwezi Disemba mwakani .
Asilimia 2.8 ya wakenya tayari wamepokea chanjo ya astarzeneca kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili ,idadi kamili ya watu waliopokea chanjo kiakmiifu ikiwa ni 754,542.
Kufikia sasa wafanyakazi wa afya 127,457 wamepokea chanjo kikamilifu Mafisa wa usalama 61,974, watu wenye umri wa miaka 58 na zaidi 229,699 , walimu 111,805, na idadi ya watu 223,607 kutoka kwa uma wakiwa wamepokea chanjo kufikia sasa .