Connect with us

Habari

KENAFF Yazindua Mikakati ya Kukabili Baa la Njaa

Published

on

Wakuu kutoka KENAFF, viongozi serikalini pamoja na wale wa kigeni katika hafla ya kuzindua mikakati ya kukuza sekta ya Kilimo nchini

Shirika la kitaifa la wakulima nchini (KENAFF) limezindua mikakati maalum mwaka 2022-2026,lengo lake likiwa kubadilisha na kukuza sekta ya kilimo kwa ajili ya kukabili baa la  njaa,kuboresha kipato na riziki bora kwa wakulima hususan wakati huu wa mabadiliko  ya tabia nchi.

Ili kufanikisha hilo,KENAFF imeainisha nguzo saba ikiwemo kuimarisha mafunzo na ushauri kwa wakulima,utetezi, na utekelezaji wa sera, kuimarisha huduma za wanachama na kuchangia katika maendeleo yao na vilevile kuboresha mfumo wa chakula nchini kenya.

Aidha nguzo zingine ni kutambua uvumbuzi na maarifa ya vijana na wanawake ili kuboresha biashara, ubunifu na teknolojia ya habari na mawasiliano katika kilimo na kukuza matumizi ya data.

Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa mikakati hiyo katika makao makuu ya shirika hilo eneo la Thogoto kwenye kaunti ya kiambu,afisa mkuu mtendaji daniel mailutha ,alisema wana matumaini ya  kuinua mamilioni ya wakulima  kujenga maisha bora kwa familia zao kulingana na matarajio ya dira(vision 2030).

‘’Kupitia mpango huu, tunanuia kuinua mamilioni ya wanachama wetu,  azimio kuu likiwa kujenga maisha bora kwa familia zao kulingana na matarajio ya dira ya 2030.tunalenga kufanikisha hili kupitia ushirikiano kati ya taasisi mbali mabili, wakulima na wataalamu katika sekta ya kilimo.’’alisema Daniel.

Mwenye kiti wa kitaifa kutoka shirika hilo Kaburu Ribu alisema kwamba mpango huo utahakikisha  vipengele vyote muhimu vya mabadiliko ya sekta ya kilimo na mikakati wa ukuaji  vinakuzwa.

‘’Mtazamo wa kenaff utakuwa kwenye  uhamasishaji na usajili wa wakulima katika biashara ya ukulima; kuimarisha  mtandao wa kutathmini thamani ya bithaa  na data za wakulima na kuwapa wakulima uwezo na ujuzi kupitia mafunzo. ‘’kaburu alisema.

kwenye hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mikakati hiyo,, naibu mkurugenzi mwandamizi wa utafiti na maendeleo kutoka  KEFRI Dkt Jane Njuguna alisema, “naipongeza kenaff kwa kujitolea kuhamasisha na kuwaandaa wakulima kote nchini kwa ajili ya uzalishaji bora. ni ombi langu  kwa wadau wengine wote katika sekta ya kilimo  kuwashirikisha wakulima kupitia mashirika yao.

Akizungumza kwa niaba ya wizara ya mazingira na misitu nchini ,dkt Jane aliongeza kuwa serikali inapania kuwashirikasha vijana kutoka sehemu mbali mbali katika upanzi wa miti kwa kuwapa miche bila malipo.

(kush:Mwenyekiti  Kaburu Ribu,kati:Dkt Jane Jjuguna kul:mkuu Daniel mailutha)

Shirika la KENAFF vile vile linatazamia kupanda miti bilioni kumi katika miaka kumi ijayo kwa ushirikiano na wakulima katika kaunti zote.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na washikadau mbalimbali ikiwemo ubalozi wa afrika kusini,israeli,uholanzi miongoni mwa wengine,ambao walishiriki katika upanzi wa miti nje ya makao makuu ya shirika hilo.

Baadhi ya wageni wakishiriki zoezi la upandaji Miti

Ignatius Openje
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *