Connect with us

Habari

Kasisi Awasilisha Kesi Ya kutaka Wahubiri Kuwa na Digiri

Published

on

Kasisi wa kanisa la United Methodist Church East Africa Bishop Daniel Wandambula aliwasilisha ombi kotini la kuwataka wahubiri kuwa na shahada kabla ya kuruhuswa kuhubiri madhabauni.

Akizungumza katika kongamano la wahubiri katika Kaunti ya Mombasa Wandambula alidai kuwa baadhi ya wahubiri wanatumia mafunzo ya bibilia kuwapotosha wafuasi wao.

Mjadala kuhusu kudhibiti makanisa liliibuka baada ya mhuburi tatanishi kutoka kanisa la Good News Internationa Paul Mackenzie kuwarai wafuasi wake kufunga hadi kufa. Zaidi ya miili 420 zimefukuliwa tangu kesi hiyo kuanza.

Katika masharti mapya iliyotolewa na serikali kila mhubiri anahitajika kuwa na cheti cha mafunzo ya theolojia, cheti cha nidhamu( certificate of good conduct)

Tayari baadhi ya makanisa yamefungwa kama kanisa la Good News Internation inalomilikiwa na Paul Mackenzie, New life prayer centre inayomilikia na Ezekeil Odero.

Charity Kilei
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *