Mwanaume mmoja kwa jina Williamson Omworo alishtaki kampuni ya kutengeneza Kondomu (Beta Health care), Shirika la kukusaya ushuru (KRA) , Mamlaka ya kudhibiti ubora wa bidhaa nchni (KEBS )kwa madai kwamba mpira wa kondomu ulipasuka wakati wa kushiriki tendo la ndoa, hatua hiyo ikimsababishia kupata ugonjwa wa zinaa.
Williamson aliishangaza mahakama baada ya kufikisha mpira uliotumika mahakamani kama ushahidi wa kipekee. Alitoa madai kwamba mashirika yaliyotajwa yalifeli katika kudhibiti ubora wa bidhaa hiyo.
Jaji Justice Mugambi alitupilia kesi hiyo kwa ukosefu wa ushahidi tosha. Jaji huyo alisema ni vigumu kudhibitisha iwapo mpira huo wa kondomu ulitumika.
Jaji Mugambi vile vile alisema kesi hiyo haiwezi kudhibitishwa kwa sababu mwanamke aliyedaiwa kujamiana na Omworo alifeli kutoa ushahidi.
Ushahidi pia ulitolewa kwamba omworo anatabia ya kushiriki tendo la ndoa na wanawake wengi ilhali ana mke.