Aliyekuwa waziri wa fedha Henry Rotich na washukiwa wengine wanne wameshtakiwa upya katika katika kashfa ya mabwawa ya Aror na Kimwarer.
Rotich amefikishwa mahakamani hii leo pamoja na David Kipchumba Kimosop, Kennedy Nyakundi Nyachiro, Jackson Njau Kinyanjui na Titus Muriithi .
Hii ni baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin haji kuondoa mashtaka dhidi ya watuhumiwa kati yao ikiwemo katibu katika wizara hiyo Kamau Thugge ambaye sasa atakuwa shahidi muhimu wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo.Thugge sasa atatoa ushahidi dhidi ya bosi wake wa zamani henry rotich.
Walipowasili mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya kupambana na ufisadi douglas ogoti, watano hao walishtakiwa kwa kula njama ya kulaghai, kushindwa kwa makusudi kutii sheria za ununuzi, kushiriki mradi bila mipango ya awali, matumizi mabaya ya ofisi na kutenda kosa la utovu wa nidhamu wa kifedha. Walikana mashtaka dhidi yao.