Visa vya kupotea kwa baadhi ya vijana katika msimu wa maandamano nchini Kenya vimeripotiwa mtaani Kibera.Familia mbili zinawatafuta wapendwa wao waliopotea tarehe 2 Agosti.Wiki tatu baadaye hawajulikani waliko huku pikipiki waliyokuwa nayo siku ya kupotea ikisalia katika kituo cha polisi cha Kibera.Uchunguzi wa kisa hiki unaendelezwa na kituo cha polisi cha Lang’ata.
Sikiliza taarifa hii iliyotayarishwa na Mwilwatsi John.