Connect with us

Fact checking

Fahamu Umuhimu wa Kupata Chanjo ya Covid19

Published

on

Chanjo nyingi dhidi ya magonjwa yanayoletwa na virusi zinaweza  kupunguza maambukizi.Hii, ni kulingana  na  shirika la  Usimamizi wa chakula na dawa nchini marekani

Kwa Mujibu wa Wataalam Kutoka Shirika Hilo, wanasayansi waliangalia maambukizi baina ya watu ambao walipokea chanjo ya pzifer ya virusi vya corona na kisha baadaye kuambukizwa. Wanasayansi hao walipata baadhi ya virusi vinavyoonyesha kuambukiza kuwa chini kwa wagonjwa walioambukizwa baada ya jaribio la kwanza ikilinganishwa na wale bado hawajachanjwa.

Hii inadokeza kwamba chanjo inaweza kupunguza msambao na pia kuathiri kuenea kwa virusi vya corona.

Majaribio ya chanjo za moderna na Oxford Astrazeneca lilionyesha kwamba inawezekana chanjo hizo zitazuia watu kuambukizwa kabisa lakini thibitisho zaidi linahitajika.

Hata Hivyo, Wahudumu wa afya wanashauri watu kuvaa  barakoa  na kudumisha umbali  hata baada ya kupata chanjo ili kuzuia maambukizi zaidi katika jamii. Mfano mwingine wa chanjo ni ile ya homa ya mafua ambayo kuna uwezekano  mdogo kwa watu walioipokea  kupata homa au kueneza homa ya mafua katika jamii.

Editor
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *