Mama akitekeleza mpango wa kangaroo Mother Care (Picha kwa Hisani)
Tangu kuanzishwa nchini kenya,mpango wa kangaroo mother care umesaidia maelefu ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati hasa mashinani. Mbinu hii ambayo humuwezesha mama kumfunga mtoto kifuani,husaidia kupata joto kama ile ya nasari,ili mtoto kuongeza uzani kwa haraka. Mpango huu hutumika kwenye hospitali zilizo na uhaba wa nasari. Hata hivyo akina baba maeneo ya magharibi mwa kenya sasa wanawasidia akina mama kupeana huduma hii ya kangaroo hospitalini na hata nyumbani,licha ya eneo hilo kuzingatia utamaduni wa hali ya juu. Mwanahabari wetu victor moturi,ametuandalia taarifa ifuatayo.