Maambukizi ya virusi vya Corona yamebainika kuwa yanachangia kulemaza mzunguko wa damu mwilini.Tafiti zilizofanywa zimebaini kua kuganda kwa damu hutokea kwenye mishipa ya damu na hivyo basi kuhatarisha hata zaidi maisha ya wanaougua gonjwa la korona.
Kulingana na utafiti uliofanywa katika mataifa ya Uholanzi na Ufaransa,asilimia 20-30 ya wagonjwa wa korona walikua na mgando wa damu katika mifumo ya usambazaji damu mwilini ambayo ni Hatari, hii huenda ikawa taswira sawa nchini Kenya.
Hali hii , kwa mujibu wa madaktari, huchangia mkurupuko wa upele mwilini , kufura kwa miguu na hata wakati mwingine Kifo.
La kutia hofu, kwa kiwango Fulani ni pale watoto wanaougua korona ,hupata matatizo ya moyo ,mapafu na akili.
Aitha ,tafiti hizo pia zinaashiria kuwepo ushahidi wa watu wazima wanaougua korona kua na matatizo ya moyo,jambo ambalo husababisha madhara makubwa ya moyo.
Wataalam wa afya wanasema hayo yanaweza epukika tu kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kutumia maji yanayotiririka na kuepuka mikusanyiko ya watu.
Zoma Zaidi taarifa hii hapa