Connect with us

Habari

Covid-19 Yabwaga Wasanii Kibra

Published

on

Geoffrey Omenta anayefahamika na wengi kama Omentality ni Msanii chipukizi kutoka mtaani Kibra

Janga la korona limeathiri pakubwa sekta mbali mbali nchini tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza mwezi machi mwaka jana. Sekta ya burudani ikiwa miongoni mwa sekta ambazo zimepata pigo .

Geoffrey Omenta anayefahamika kwa jina la usani la omentality ni mwanamziki chipukizi kutoka eneo bunge la kibra katika mtaa wa 42 .

Omentality ni miongoni mwa wasanii ambao wamelazimika kutafuta njia mbadala ya kujikimu kimaisha kutokana na athari za janga hilo.

Kabla ya corona, wasanii wengi walikuwa wanategemea tamasha za mziki na kuburudisha katika sherehe ili kujipatia kipato.
Agizo la rais la kufunga vilabu pamoja na vyumba vya burudani na hata kafyu ilizima milango ya ajira ya wasanii kama omentality.

“Nililazimika kufungua duka ili kuuza bidhaa rejareja kwasababu usanii haulipi kwa sasa” alisema Omenta.

Mbang’a Amechoma ni wimbo aliouzindua mwezi jana

Wasanii wengi ulimwenguni, kwa kiwango kikubwa, hutegemea youtube ili kujipatia kipato kadri nyimbo zao zinavyosikika. lakini kwa omentality, hilo haliwezekani kwani hajapata umaarufu bado.

licha ya hayo, Geoffrey hajakataa tamaa ya kuwa msanii mashuhuri hapa nchini na imani kuwa janga la covid19, kama magonjwa mengine ya hapo awali, litakabiliwa vilivyo.

Jackline Mokabi
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *