Rais wa Marekani Joe Biden amelionya Kundi la Taliban dhidi ya kushambulia vikosi vya Marekani vinapoendelea kuendesha oparesheni ya kuondoka na kuondoa wanadiplomasia wake nchini Afghanistan .
“Naweka wazi kwa Taliban , ikiwa watahilafiana na oparesheni yetu uwepo wa Marekani utajibu kwa vishindo “ alisema Biden kwenye hotuba yake kwa wandishi wa habari Jumatatu Agosti 16 2021 ,
Akizungumza kwenye ikulu ya white house bada ya Kundi la Taliban kunyakua Kabul mji mkuu wa Afghanistanna kuigia kwenye ikulu ya rais , Biden amesisitiza kuwa walifanya kila wawezalo ikiwemo kulipa mafunzo ya kijeshi jeshi la Afghanistan lenye takriban wanajeshi 300,000 na vifaa vya kijeshi pamoja na kulipa mishahara yao.
Biden pia amenyoshea kidole cha lawama wapinzani wake hasa mataifa ya Urusi na China kwa kile amesema kuwa walifurahia kuona Marekani ikiendelea kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa taifa la Afghanistan .
Rais biden hata hivyo amesema kuwa hajuitii uamuzi wake wa kuondoa majeshi ya marekani nchini humo. Ashraf Ghani ambaye ni rais wa taifa hilo alitoroka kwa kile alichosema kuwa alizuia umwagikaji wa damu .
Viongozi mbalimbali kote duniani wamekuwa wakikosoa uamuzi wa Biden wa kuyaondoa majeshi ya MarekanI nchini Afghanistan swala ambalo limesababisha kundi la Taliban kuchukua umiliki wa nchi hiyo kwa mara nyingine.
Kundi la Taliban liliondolewa madarakani na vikosi vilivongozwa na majeshi ya Marekani mwaka wa 2001 na limedumu humo nchini kwa miongo miwili sasa . Taliban imesema kuwa kila kitu ki shwari na kutoa hofu iliyoko kuwa watakandamiza watoto na wanawake . kumekuwepo na hofu kuwa wanawake walio nchini afganistan hawataruhusiwa na kundi la Taliban kuendelea na mmasomo yao .