Connect with us

Habari

Biba; Kenya Haiko Tayari Kwa Mahindi Ya GMO

Published

on

Daniel Maingi,Ann Maina,Wanjiru Kamau wakihutubia Wanahabari Hoteli ya Golden Tip. PICHA(Ignatius Openje)

Muungano wa usalama wa viumbe hai nchini,maarufu Biodiversity and Biosafety Association of Kenya,umeshutumu vikali hatua ya serikali ya hivi punde ya kuagiza gunia milioni  kumi za mahindi ya kijenetiki GMO.

Akizungumza katika hafla ya mafunzo kwa wanahabari kuhusu bidhaa za GMO na ukulima kwa jumla,mratibu wa kitaifa kutoka shirika hilo Ann maina,amesema bidhaa hizo zina madhara kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa saratani na uvimbe wa ubongo maarufu brain tumor.

Maina amedokeza kuwa serikali imeshauriwa  na matapeli kutoka mataifa ya nje, wanaolenga kupata faida kwa kuuzia wakenya bidhaa za GMO ambazo ni hatari.

Anasema iwapo bidhaa hizo zitatumiwa,madhara yake huenda  yakaanza kutokea baada ya miaka minne.

“Baadhi ya watafiti wanatilia shauku bidhaa za GMO baada ya utafiti kuonesha wale wanyamba ambao walitumiwa katika majaribio ya bidhaa kama mahindi na viazi na bidhaa zingine ambazo zinalengwa kununuliwa na serikali,ziliwafanya wanyama ikiwemo panya  kuwa na brain tumor ishara tosha kwamba vyakula hivyo vina shida.Vyakula vinvyozalishwa kijenetiki vinaweza kusababisha aina mbalimbali ya kansa ikiwemo ya damu,matiti,shida za uzazi na mishipa.Sasa ikiwa wanasayansi wana tashwishi kwa GMO,mbona Serikali inataka kuwaumiza wakenya?”Alifoka Maina.

Wakati uo huo Mwanasayansi wa Kilimo na Bayolojia Daniel Maingi kutoka shirika la kuangazia maswala ya vyakula yaani Food Rights Alliance,ameeleza hofu yake kwamba wakulima watajipata katika hali ngumu  iwapo mbegu za kijenetiki zitapandwa,kwani huenda zikachanganyikana na mbegu za kiasili shambani.

Maingi badala yake amependekeza serikali kukumbatia kilimo hai kama lilivyopendekeza shirika la afya ulimwenguni WHO.

“Kuna ule mchanganyiko ambao hutokea maarufu pollination ,kwa mfano sisi tunataka kupanda mbegu za kienyeji na jirani anapanda GMO,ile pollen inaruka kutoka hii mbegu inakuja hii ingine,sasa wakulima wakidhani  mazao ni ya kienyeji wanakuta  kumbe ni ya GMO jambo ambalo litawafanya kupoteza ile mbegu yao ya kiasili.Tumesikia WHO ikishinikiza mataifa yafanye bidii kuhakikisha chakula hakijazalishwa kijenetekin na madawa ya Roundup na Glyphoset ambayo yanasababisha saratani.”Alisema Maingi.

Wanjiru Kamau mtaalam wa sera na utetezi kwa upande ameitaka serikali pamoja na wazalihsaji na wasagaji kuhakikisha pakiti zote za bidhaa za GMO zinatofautishwa kwa kuwekewa majina maalum tofauti na bidghaa za kiasili ili wakenya wawe na fursa ya kujiamlia bidhaa wanayopeendelea.

Oktober tarehe tatu mwaka huu Baraza la mawaziri liliafikia kuondoa marufuku ya bidhaa hizo kama njia moja wapo ya kupungunguza makali ya njaa yanayothiri mamilioni ya wakenya kutokana na ukame unaoshuhudiwa Nchini Kenya kufuatia mabadiliko ya tabia Nchi.

Ignatius Openje
+ posts
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *