Wakazi wengi wa mtaa wa Kibra hutupa taka zao ovyo kutokana na ukosefu wa njia mwafaka za kuondoa taka mtaani. Nyingi ya taka hizi za mabaki ya vyakula, makaratasi, sodo zilizotumika na kwa wakati mwingine nepi. Uchafu huo hutupwa mitoni na vile vile kwenye mitaro ya majitaka. Hali hii husababisha mafuriko ya ghafla kila kunaponyesha na kupelekea hasara na hata vifo wakati mwingine. Mwanahabari wetu Alex Kememwa amechambua takwimu muhimu zinazoonyesha tatizo la mafuriko mtaani Kibera katika makala yafuatayo.