Mbunge wa Embakasi Mashariki Paul Ongili, almarufu kama Babu Owino, ameeleza imani yake ya kunyakua kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi kwenye uchaguzi mkuu mwaka wa 2027.
Kulingana na Babu Owino, ana kila anachohitaji kumpiku gavana Johnson Sakaja kwenye uongozi wa kaunti ya Nairobi.
“ Gavana Sakaja anapasha hicho kiti moto, angalia bunge la kitaifa sasa, angalia magavana, angalia maseneta, angalia woman Reps na MCAs….kuna aliye bora kuliko Babu Owino hapo? Sijisifu, niambie tu,” Babu alisema haya kwenye mahojiano wa matandao wa YouTube kinachotambuliwa kama ‘Convo Unscripted. “Naweza kukuambia, 101%. Yeye (Sakaja) nikishika nafasi tu…Sakaja amewekwa hapo ili kunisafishia njia.”
Babu Owino anahudumu kwa muhula wa pili kama mbunge wa Embakasi mashariki na amezidisha umaarufu miongoni mwa vijana.
Kabla ya kujitosa katika siasa za kitaifa babu Owino alihudumu kwa muda kama mwenye kiti wa muungano wa wanafunzi (SONU) chuo kikuu cha Nairobi.