Serikali inakusudia kuondoa chanjo ya covid-19 kutoka kaunti zinazopena chanjo hiyo kwa kasi ya chini na kuisambaza tena kwa mikoa mingine inayoathirika zaidi.
Akihutubia wanahabari hii leo , waziri wa afya mutahi kagwe amesema takriban dozi laki 2 zinalengwa kuondolewa kutoka kaunti hizo kutokana na idadi ndogo ya usambazaji wa chanjo huku akisisitiza kuwa serikali haitakubali chanjo kuharabika.
Akizungumza katika kaunti ya nyeri , waziri kagwe amesema hadi kufikia sasa takriban wakenya laki tisa wamepokea chanjo hiyo kote nchini.
Wahudumu wa afya wapatao elfu mia moja sitini,mianne sitini na nane,walimu elfu mia moja arobaini na mbili,mia sita ishirini na nne na maafisa wa usalama elfu sabini na sita miatano sabini na nane ni miongoni maw wale wamepokea chanjo.