Mfanyibiashara mmoja wa kiume ameuwawa na majambazi asubuhi ya leo katika eneo la kichinjio. Kulingana na mashuhuda, majambazi hao wawili walimuibia pesa mfanyikazi huyo katka duka lake na kisha kumpiga risasi na kuondoka,
Polisi walifika katika eneo la mkasa dakika chache na kupata majambazi hao wametoroka. Mfanyibiashara huyo alikimbizwa katika kituo cha afya cha Kibera D.O na baadaye akafariki kutokana na majeraha.
Msako wa Kuwatafuta majambazi hao unaendelea. Hayo yanajiri huku wananchi wakizitaka asasi za usalama mtaani Kibra kukabili ongezeko la visa vya wizi vilivyoongeza katika siku za hivi karibuni.