Visa vya dhulma za Kijinsia vimeonekana kukuthiri mtaani Kibra. Cha hivi punde kinamhusisha mwanamke wa umri wa makamu ambaye bado anatafuta haki baada ya kuchomwa na aliyekuwa mpenziwe wa zamani.
Mwanamke huyo ambaye tumebana jina lake kwa sababu za kiusalama amesema aliyekuwa mumewe alimdanganya kwa kumwalika kwa sherehe za kufungua Mwaka. Mwanamke huyo alikubali wito wake na kumfuata nyumbani kama alivyoahidi.
Mwanaume huyo alimwacha kwenye nyumba kwa muda kisha baadae akarejea na kuanza vurugu huku akimshutumu kwa kutokuwa mwanifu katika penzi lao.
Baadae,alimpiga kwa kutumia stovu huku akiumwagilia mwili wake mafuta taa na kisha baadaye kusababisha majeraha yaliyotokana na moto aliouwasha .